Baada ya kutaka Netanyahu akamatwe, ICC nayo yawekewa vikwazo na Marekani
Eric Buyanza
June 5, 2024
Share :
Bunge la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kupitisha sheria ambayo itaiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya mwendesha mashtaka wake kuomba hati ya kukamatwa kwa maafisa wa Israel.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya The Hague kusema kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant wanapaswa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na vita huko Gaza.
Mwendesha mashtaka pia anatafuta vibali vya kukamatwa kwa viongozi watatu wa Hamas.
Mswada huo uliopendekezwa na Warepublican wanaounga mkono Israel, unalenga maafisa wa ICC waliohusika katika kesi hiyo kwa kuwazuia kuingia Marekani.