pmbet

Baada ya kuzoa tuzo za Grammy Eilish abeba tena Oscar

Sisti Herman

March 11, 2024
Share :

Baada ya kuondoka na Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka katika Tuzo za Grammy 2024 na sasa mwanamuziki Billie Eilish, ameshinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka katika Tuzo za Oscar 2024.

Wimbo huo uitwao ‘What Was I Made For’ ambao unasikika kwenye filamu ya ‘The Blockbuster Barbie’ kwa mwaka 2024, tayari umepata tuzo mbili kubwa nchini Marekani, ambapo mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 116, katika mtandao wa YouTube ukiwa na miezi 8 tangu kuachiwa kwake.

Billie Eilish, anatamba na ngoma zake kama Lovely, Bad guy, Ocean Eyes, Bury a friend na nyinginezo.

Huu unakuwa wimbo wa pili kushinda Tuzo ya Wimbo Bora wa mwaka huku wimbo wa kwanza kutoka katika filamu kushinda tuzo hiyo ukiwa ni ‘My Heart Will Go On’ kutoka katika filamu ya Titanic, ulioimbwa na Celine Dion

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet