Baada ya miaka 10 Rihanna abadili Profile Picture instagram
Joyce Shedrack
April 23, 2024
Share :
Msanii wa mziki, mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Duniani kutoka nchini Barbados mwenye umri wa miaka 36 Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna amezua gumzo baada ya kubadilisha profile picha kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyodumu kwa miaka kumi.
Rihanna ambaye mwanzo alikuwa ameweka profile picha ya kimdoli kwa sasa ameibadilisha baada ya kupita miaka kumi na kwa sasa ameweka picha ya mkono wa mtu ulioshika kitu kinachonga'a.
Mwanadada huyo aliyejizoelea umaarufu mkubwa duniani kupitia nyimbo zake za kuvutia kama We found Love, Umbrella na Lift Me Up kwa sasa ameacha kufanya mziki na kujihusisha na biashara zaidi.
Kwa sasa imepita takribani miaka 9 tangu Rihanna aachilie album yake ya mwisho ya Anti aliyoitoa mwaka 2016.
Wewe inakuchukua muda gani kubadilisha profile picha yako ?