Baada ya miaka 30: Aliyepanga mauaji ya Tupac apatikana
Eric Buyanza
September 1, 2026
Share :

Aliyekuwa kiongozi wa genge la uhalifu, Duane "Keffe D" Davis, amekutwa na hatia ya kupanga mauaji ya aliyekuwa mwanamuziki wa Hiphop, Tupac Shakur – ikiwa ni miaka 30 sasa baada ya tukio hilo.
Uamuzi huo wa kihistoria umetolewa jana na Baraza la wazee wa mahakama baada ya mashauriano yaliyochukua muda wa saa tatu. Huyu ndio mtuhumiwa wa kwanza kabisa kupatikana na hatia ya jinai tangu mauaji hayo yatokee mwaka 1996.
Akiwa amevaa suti nyeusi, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 63 alisimama bila kuonyesha hisia zozote mahakamani huko Las Vegas wakati hukumu ikisomwa, kabla ya kusema kuwa atakata rufaa.
Ndugu wa 2Pac walionekana wakiwa wameshikana mikono, huku baadhi yao wakikumbatiana na kulia.
2Pac alikuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa rap duniani, na aliuawa akiwa na umri wa miaka.





