Baada ya miaka 58, kituo cha afya chapata gari la wagonjwa
Eric Buyanza
February 27, 2024
Share :
Kituo cha afya Magubike kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, chenye miaka 58 tangu kilipoanzishwa mwaka 1966, hatimae kimepata gari la wagonjwa (Ambulance).
Mbunge wa kilosa, Prof. Palamagamba Kabudi ndiye aliyekabidhi gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 170 ikiwa ni jitihada za serikali katika kuboresha utoaji wa huduma kituoni hapo.
Kituo hicho kinachohudumia takribani kata sita awali kilikuwa kikitumia gari ndogo katika kutoa huduma hiyo jambo ambalo lilikuwa halikidhi mahitaji katika kuhudumia wananchi hasa huduma ya mama na mtoto.