Baada ya Msiba wa Gardner, Malkia Karen afunguka
Sisti Herman
April 29, 2024
Share :
Mwanamuziki Malkia Karen amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwenye msiba wa Baba yake mzazi aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Gardiner Habash.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram (Insta story), Karen ameandika:
“Kipekee nitoe shukran za dhati sana kwenu nyote kwa salamu za pole na za faraja Mwenyezi Mungu akawe nanyi. Tuendelee Kumuweka kwenye Maombi Mpendwa wetu Apumzike kwa Amani.”
Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mtangazaji huyo alipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.