pmbet

Baada ya Ronaldo, ni zamu ya Messi sasa kukutana na Trump Ikulu

Eric Buyanza

February 28, 2026
Share :

Lionel Messi na klabu yake anayochezea ya Inter Miami wamealikwa ikulu ya Marekani (White House) tarehe 5 machi 2026, kusherehekea ubingwa wao wa Ligi kuu ya soka nchini Marekani (MLS Cup 2025).


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Messi kutembelea Ikulu ya Marekani, ingawa alipewa Medali ya Uhuru ya Rais (Presidential Medal of Freedom) Januari 2025, lakini hakushiriki kwenye sherehe hizo.

Hii inafuatia ziara ya Cristiano Ronaldo Ikulu Novemba 2025, ambapo alikutana na Rais Donald Trump kwa mualiko wa chakula cha usiku.


Ni desturi kwamba timu iliyoshinda ubingwa hualikwa kwenye Ikulu ya Rais.
Columbus Crew ilikuwa timu ya mwisho ya MLS kupokea mwaliko huo mwaka wa 2024.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet