Baada ya Simba, Yanga kuwavaa JKT Tanzania kesho
Sisti Herman
April 22, 2024
Share :
Baada ya 'kuwanyoa' 2-0 watani zao Simba, klabu ya Yanga kesho jioni itashuka kwenye dimba la Meja Jen. Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam kuwavaa klabu ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Yanga wanaoongoza msimamo wa ligi watachuana na JKT iliyopo nafasi YA 15 kati ya timu 16.