Baada ya Waziri Mkuu kutimuliwa, Spika nae atangaza kujiuzulu
Eric Buyanza
May 25, 2026
Share :

Spika wa Bunge la Senegal ametangaza kwamba atajiuzulu wadhifa huo siku mbili baada ya mshirika wake wa karibu Ousmane Sonko kuvuliwa uwaziri mkuu, hatua inayozidisha mzozo wa kisiasa nchini humo.
Uamuzi huo wa spika El Malick Ndiaye unamfungulia njia Sonko kuwania nafasi hiyo ya kuliongoza bunge linalodhibitiwa na chama chake cha Pastef ili kumkabili Rais Basirou Diomaye Faye.





