pmbet

Baada ya Wembley, Endrick afunga tena Santiago Bernabeu

Sisti Herman

March 27, 2024
Share :

Kinda mpya wa Real Madrid na timu ya taifa Brazil Endrick mwenye umri wa miaka 17 anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye viwanja vikubwa viwili mfululizo baada ya jana kuifungia Brazil goli moja kwenye sare ya 3-3 dhidi ya Hispania.

Endrick ambaye alifunga siku tatu zilizopita dhidi ya Uingereza kwenye dimba la Wembley amefunga tena dhidi Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, mmoja kati ya viwanja vya nyumbani vya timu ya Taifa ya Hispania unaomilikiwa na klabu ya Real Madrid ambayo pia ni klabu atakayoanza kuitumikia kuanzia msimu ujao.

 

Baada ya kufunga bao hilo Endrick alienda kushangilia na baba yake mzazi ambaye alikuwa jukwaani kumshuhudia.

Kwenye sare hiyo, mabao mengine ya Brazil yalifungwa na Rodrigo na Lucas Paqueta huku ya Hispania yakifungwa na Rodri na Dani Olmo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet