pmbet

Baadhi ya vituo vya kulea watoto yatima vyatuhumiwa kutafuna misaada

Eric Buyanza

January 5, 2024
Share :

Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) na vituo vya kulelea watoto yatima yanadaiwa kujinufaisha kwa fedha za misaada inayotolewa na wahisani kusaidia watoto hao.
 

Madai hayo yametolewa na Mkuu wa Idara ya Falsafa na Maadili,Chuo Kikuu cha Mtakafifu Agostino (SAUT) Mwanza,Padri Dkt.Innocent Sanga,wakati wa chakula na watoto yatima kilichotolewa na BAKWATA mkoani humo ilishirikiana na Rocky Solution Ltd.
 

Akizungumza kabla ya chakula hicho Padri Dkt.Sanga amesema baadhi ya NGO’s na vituo vya kulelea yatima vinawatumia watoto hao kibiashara na kujinufaisha kwa fedha za misaada inayotolewa na wahisani.
 

Amesema serikali katika kukomesha tabia hiyo itunge sera ya kuvipata vituo vya kuwalea,kuwatetea na kuwalinda yatima pamoja na kutengeneza mifumo ya kuwabaini katika vitongoji,vijiji na mitaa.
 

“Tahadhari,serikali yawezekana inaogopa, baadhi ya NGO’s na vituo vya watoto yatima vinawatumia kibiashara na kujinufaisha,wanawafanya kama bidhaa na wanakula fedha zao baada ya kuandika maandiko ya kuomba fedha kwa wahisani,”amesema Padri Sanga.
 

Ameishauri serikali kuhakikisha vituo na mashirika hayo yanasajiliwa,ufanye uratibu na ufuatiliaji kwa wanaojinufaisha kwa fedha za yatima na kuwachukulia hatua za kisheria.
 

“Tumewakandamiza yatima kwa njia mbalimbali,Tanzania imegeuka janga kubwa la yatima kudhulumiwa,kuonewa na kunyang’anywa mali zao na ndugu,hivyo tutafakari dhambi hii na kutubu,”amesema Padri Dky.Sanga.
 

Mkuu huyo wa Idara ya Falsafa na Maadili ya chuo cha SAUT Mwanza,pia ameishauri serikali itenge bajeti ya kuwasaidia yatima kupata elimu na miongoni mwao wana uwezo mkubwa kiakili.
 

Pia amesema changamoto ya watoto yatima kukimbilia mitaani ni matunda ya kutukanwa na kukandamizwa na ndugu zao ili kuwaepuka maadui hao wanaowakamindamiza wakihofia usalama wao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet