pmbet

"Baba alichoma moto Bilioni 5, ili kumpa joto dada yangu"

Eric Buyanza

January 11, 2024
Share :

KWA TAARIFA YAKO: 'Mfalme wa cocaine' Pablo Emilio Escobar Gaviria (PABLO Escobar) aliwahi kuchoma moto dola milioni 2 (Bilioni 5 za kibongo) ili kumpa joto mwanae.

Hayo yalithibitishwa na mtoto wa mfanyabiashara tajiri zaidi wa dawa za kulevya katika historia ya dunia, Juan Pablo Escobar ambaye baadae alibadilishwa jina na kuitwa Sebastián Marroquín.

Katika mahojiano ya mwaka 2009 Marroquín alielezea maisha ya baba yake yalivyokuwa ambaye kampuni yake ilitoa asilimia 80 ya kokeini yote duniani na kumuingizia mapato yanayokadiriwa kufikikia $420 milioni kwa wiki.

Kulingana na Marroquín, familia hiyo ilikuwa ikiishi mafichoni kwenye milima ya Medellín wakati siku moja dada yake Manuela (binti ya Escobar) alipoumwa....na joto la mwili wake liliposhuka ndipo baba yake akaamua kuchoma moto dola milioni 2 pesa taslimu ili kumpa joto binti yake huyo.

Marroquín anasema familia yao ilikuwa ikihama makazi kila baada ya masaa 48 katika maficho 15 tofauti tofauti kwenye maeneo hayo ya Medellín kwa sababu ya kukimbia mkono wa dola.

Japo alikuwa mtu anayetafutwa zaidi kwa uharamia wa dawa za kulevya duniani, Pablo na mwanae Marroquín waliwahi kupiga picha mbele ya lango la Ikulu ya Marekani (Whitehouse) mwaka 1981 bila kutambulika.

Hadi mwaka 1993 utajiri wake ulikuwa unafikia dola za Kimarekani bilioni 30 zilizotokana na biashara hiyo haramu.

Pablo Escobar alifariki tarehe 2, Disemba mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 44, akiwa katika mji wa Medellin, Antioquia, nchini Colombia. Chanzo cha kifo chake kikiwa ni majeraha ya risasi alizopigwa kichwani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet