pmbet

Baba na watoto wake wakamatwa kwa kusaidia magaidi Urusi

Eric Buyanza

March 26, 2024
Share :

Kamati ya Uchunguzi Nchini Urusi, imeagiza kukamatwa kwa washtakiwa wengine watatu wa familia moja (baba na watoto wake wawili) ambao tayari wamefikishwa mahakamani na kujumuishwa kwenye kesi ya shambulizi la kigaidi lililoua zaidi ya watu 130 Crocus City Hall nchini humo wakidaiwa kuhusika kwa kuwasaidia magaidi hao kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kupanga mipango ya shambulizi na kuwauzia gari jeupe ambalo walitumia kufika Crocus Hall na kuwaua watu kisha wakalitumia gari hilo kujaribu kutoroka.

Washtakiwa hao ni Islomov Isroil Ibrahimovich (62) na watoto wake Islomov Aminchon Isroilovich na Islomov Dilovar Isroilovich ambao wote wamesomewa mashtaka na kupelekwa mahabusu hadi Mei 22, 2024 watakaporudi tena mahakamani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet