Baba wa Jude Bellingham aitwa kukipiga timu ya taifa ya Uingereza
Eric Buyanza
October 30, 2026
Share :

Jina la familia ya Bellingham linaendelea kuweka historia katika soka la Uingereza baada ya Mark Bellingham, baba mzazi wa mastaa wa soka Jude na Jobe Bellingham, kuitwa rasmi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza ya Wakongwe (England Veterans) wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Akiwa na umri wa miaka 50, mshambuliaji huyo wa zamani ambaye alitikisa soka la madaraja ya chini nchini Uingereza (non-league football) kwa kufunga zaidi ya mabao 700, sasa anajiandaa kupata ladha yake ya kwanza kabisa ya soka la kimataifa.
Hatua hii inamfanya Mark kuwa mwanachama wa tatu kutoka familia hiyo kuvaa uzi wa Uingereza, akifuata nyayo za wanawe, Jude Bellingham (anayeichezea Real Madrid) na Jobe Bellingham (Sunderland).
Bellingham Mzee amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kitakachoshuka dimbani Jumapili hii, Novemba 1, 2026, kumenyana na Jamhuri ya Ireland katika mchezo utakaopigwa huko Cambridgeshire.





