pmbet

Baba wa Kobe Bryant aiweka sokoni pete ya mwanae kwa milioni 358

Eric Buyanza

March 23, 2024
Share :

Joe "Jellybean" Bryant, Baba mzazi wa aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu marehemu Kobe Bryant, ameiweka kwenye mnada kwa dola $141,000 (sawa na sh milioni 358 za kibongo) pete ya Kobe Bryant ya ubingwa wa NBA mwaka 2000 alioupata akiwa na timu yake ya Lakers.
 

Pete hiyo iliyowekwa sokoni na Mzee Bryant ina karat 14 za dhahabu, pamoja na vipande 40 vidogo vya almamsi huku ikiwa na maandishi yaliyoandikwa 'LAKERS'. 'WORLD CHAMPIONS', "BRYANT" pamoja na namba yake ya jezi '8'.
 

Hata hivyo pamoja ya kwamba pete hii ina dhahabu pamoja na almasi, lakini sio yenyewe halisi kwani Kobe wakati wa uhai wake alitengeneza hii kama nakala maalum kwa ajili ya zawadi kwa baba yake na akaitunza ile original kwa ajili yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet