pmbet

Baba yangu alicheza Yanga - Kitenge

Joyce Shedrack

January 24, 2024
Share :

Mwandishi mkongwe wa michezo Tanzania Maulidi Kitenge ameweka wazi kuwa  hana timu anayoshabikia kati ya Simba na Yanga japokuwa baba yake mzazi alishawahi kuichezea klabu ya  Yanga .

Maulidi Kitenge ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na PM Tv ndani ya kipindi cha michezo cha sports gear, Kitenge amesema....

"Mimi baba yangu mzazi alicheza Yanga kama beki namba mbili sasa mawazo ya watu wanajua kwa maana baba yake alicheza yanga na yeye ni Yanga, kwahiyo mtu anaweza kusema huyu ni yanga basi na mimi nakubali " Maulidi Kitenge

Hata hivyo, Kitenge amesema alikuwa anaishabikia klabu ya Meko kabla ya kushuka daraja lakini kwa sasa timu zote mbili za kariokoo ni za kwake na yupo tayari kufanya kazi na Simba ikitokea.

Maulidi Kitenge amezipongeza klabu za Simba na Yanga kwa kuingia katika mfumo wa uendeshaji wa kisasa japokuwa kwa upande wa Simba bado haijakamilika lakini tayari wamepiga hatua .
 

Akizungumzia mchezo wa leo wa Taifa Stars  dhidi ya DR Congo, Kitenge amesema bado Tanzania tuna nafasi ya kufuzu 16 bora ni kumfunga tu DR Congo jambo linalowezekana kabisa .

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet