Baba yangu alinifanya nijione sina hela – Davido
Eric Buyanza
January 28, 2025
Share :
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, Davido amefichua kuwa mzigo alionao baba yake (Utajiri) uliwahi kumfanya ajione yeye hana hela kabisa.
Akiongea kwenye mahojiano ya hivi karibuni msanii huyo aliulizwa ni nani amewahi kumfanya ajisikie si lolote licha ya utajiri wake.
SWALI: "Katika maisha yako, umewahi kukutana na mtu ambaye alikufanya ujihisi hauna hela?"
DAVIDO: "Ndiyo, Baba yangu."
Itakumbukwa kwenye mahojiano miezi kadhaa iliyopita Davido aliwahi kusema ilimchukua miaka mingi kugundua kuwa baba yake ni mtu tajiri sana.