Babu Tale avutiwa na uwezo wa Jay Melody
Sisti Herman
May 7, 2024
Share :
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Meneja wa msanii wa WASAFI akiwemo Diamond Platnumz, Babu Tale kama ilivyo kawaida yake kupongeza wasanii mbalimbali nchini wanaofanya vizuri leo ameamka na mwanamuziki Jay melody ambapo aliamua kumsisitiza kuendelea kukaza na kuacha kusikiliza maneno ya watu.
Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare nyimbo tatu za Jay zilizokuwa katika albumu yake mpya ya ‘Therapy’ ikiambatana na ujumbe wa kuipongeza album hiyo kuwa ni kali huku akimtaka msanii huyo kuwawakilisha vyema watu wa Morogoro na endapo atataka kufanya show mkoni humo basi yeye atajitoa kwa hali na mali.
“Katika kipindi cha kazi zake za muziki nimepata kusikiliza nyimbo zake nyingi lakini kubwa zaidi nimesikiliza Album yake nzima, kwa hakika hakuna wimbo wa kupeleka mbele kwa maana zote zinamsukumo wa kusisikilizwa zaidi ya mara moja kisha unafuata nyingine.
Nakukaribisha ukihitaji lolote toka kwangu, milango iko wazi wakati wote. Naendelea kukuona mbali sana na watanzania wanatakiwa wajue kuwa Bongo Fleva kwa sasa inafuata mkondo wa wasilisho lako. Kaza Mwana wa ukae na ukae ukijua na mimi ni sehemu ya mashabiki wako”
Aidha kwa upande wa mwanamuziki huyo hakuliacha lipite hivi hivi aliamua kumjibu Babu Tale kupitia upande wa ‘komenti’ ambapo alimshukuru kwa nasaha zake na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Nimefurahi kujua kuwa wewe ni miongoni mwa mashabiki zangu, nashukuru pia kwa kunifungulia milango ya ushirikiano na nitaitumia hii nafasi vizuri, ni muhimu sana kwangu kufanya jambo kubwa morogoro. Nitajitahidi kuendelea kufanya mziki mzuri ili nisiwaangushe mashabiki wangu Shukran sana MH. TALE TALE” ameandika Jaymelody