Bacca anatusaidia timu ya Taifa - Msuva
Sisti Herman
December 28, 2023
Share :
Mshambuliaji na nahodha msaidizi wa Taifa Simon Msuva amesema beki wa Zanzibar Heroes na klabu ya Yanga ni mmoja kati ya wachezaji bora sana kwa sasa na amekuwa msaada kwa timu ya Taifa kwa siku za karibuni.
“Ni mchezaji mzuri, nimekuwa nikimfuatilia, anatusaidia kiukweli kwenye timu yetu ya Taifa” alisema Msuva wakati akitoa tathmini ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kufungua uwanja wa Amaan kati ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes.
Msuva pia anahusishwa kujiunga na Yanga kwenye dirisha la usajili.