pmbet

BADO MABAO 4 TU! Messi aandike rekodi ya dunia ya free-kick

Eric Buyanza

September 21, 2026
Share :

Nyota wa soka ulimwenguni na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, sasa anahitaji kufunga mabao 4 pekee ya adhabu ndogo (free-kicks) ili kuandika historia mpya kama mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi ya free-kick katika historia ya soka duniani.

 

Kwa sasa, mchezaji wa zamani wa Brazil na klabu ya Corinthians, Marcelinho Carioca, ndiye anayeshikilia rekodi hiyo ya kihistoria akiwa na jumla ya mabao 78 ya free-kick. Messi, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Inter Miami CF nchini Marekani, anashika nafasi ya pili akiwa na jumla ya mabao 75.

 

Bao lake la 75 alilifunga jana Septemba 20, 2026, kwa mkwaju safi wa adhabu katika dakika ya 24 wakati Inter Miami CF ilipotoka sare ya 2–2 dhidi ya San Diego FC kwenye ligi ya MLS

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet