pmbet

Bakari ajiua kwa kujinyonga na mtandio, kisa wivu wa mapenzi

Eric Buyanza

February 19, 2024
Share :

Mkazi wa kijiji cha majengo kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Bakari Mtepa amekufa kwa kujinyonga na mtandio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
 

Mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa na mtandio shingoni ukiwa umening’inia kwenye tawi la mti wa mkorosho.
 

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Mtaki Kurwijila amesema tukio hilo limetokea Februari 18, 2024 saa 12 asubuhi.
 

"Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata katika eneo la tukio kuna karatasi iliyokuwa imeandikwa ikielezea sababu hizo alizochokuwa marehemu kujinyonga" alisema Kamanda Mtaki
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet