Baleba atambulishwa rasmi Man United
Sisti Herman
August 25, 2026
Share :

Klabu ya Manchester United imemtambulisha rasmi kiungo wa kati Carlos Baleba kuwa mchezaji wao mpya akijiunga nao kutokea klabu ya Brighton.
Baleba amejiunga Man United kwa ada ya uhamisho ya Paundi Milioni 65 wenye nyongeza ya Paundi milioni 5 huku akijifunga mkataba wa miaka mitano hadi 2031 wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Baleba akiongea na idara ya habari ya timu hiyo alisema “Ni hisia ya ajabu kujiunga na klabu ya ndoto zangu. Sina subira ya kufanya kazi na Michael Carrick; uzoefu na maarifa yake yanamfanya kuwa kocha mwafaka kabisa kunisaidia kufikia kiwango cha juu zaidi.”





