pmbet

Baltasar Engonga ahukumiwa miaka 18 jela.

Joyce Shedrack

July 3, 2025
Share :

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha la Equatorial Guinea, Baltasar Engonga Ebang amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa kosa la ubadhirifu wa fedha za uma na tuhuma za rushwa.

Baltasar Engonga

Baltasar alipata umaarufu mwishoni mwa mwaka 2024 baada ya video zake za ngono kusambaa kwenye mitandao ya kijamii licha ya kuwa ni baba wa watoto sita huku akiwa amefunga ndoa na mwanamke mmoja.

 

Tangu kipindi hiko amekuwa akikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha kutokana na ulaghai wake wa usimamizi wa kampuni inayomilikiwa na serikali chini ya Wizara ya Fedha.
 

Baada ya ushahidi kukamilika siku ya jana Jaji wa Mahakama Kuu ya Nchi hiyo ametangaza hukumu hiyo ya miaka 18 jela.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet