Banda ashinda kesi FIFA, wasauzi kumlipa milioni 360
Sisti Herman
March 13, 2025
Share :
Baada ya kushindwa kumlipa Tsh Million 360 beki Mtanzania Abdi Banda, klabu ya Richards Bay FC ya Afrika Kusini imefungiwa kufanya usajili na Shirikisho la soka Duniani (FIFA).
Awali Shirikisho hilo lilitoa siku 45 kwa klabu kumlipa Banda, hivyo baada ya kupitiliza siku hizo bila malipo, rasmi wamethibitisha katika barua yao mpya kuwapiga kibano hicho Richards Bay.
Ikumbukwe mlinzi huyo ambaye sasa anachezea Dodoma Jiji alishinda kesi baada ya klabu yake hiyo ya zamani kukiuka makubaliano ya mkataba.