Baraza kocha mkuu Pamba
Sisti Herman
July 15, 2025
Share :
Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu za Biashara utd ya Mara, Kagera Sugar na Dodoma Jiji, Francis Baraza ameripotiwa kurejea nchini kukinoa kikosi cha wana Tp Lindanda Pamba Jiji ya jijini Mwanza.
Kocha huyo raia wa Kenya ana sifa ya kuvipa vipaji chipukizi jukwaa la kuonesha uwezo wao mfano ni kama Denis Nkane na Novatus Dismas wakiwa Biashara utd ya Mara.