Barbara kurejea Simba, apishana na Kajula
Sisti Herman
June 5, 2024
Share :
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Barbara Gonzalez kurejea kwenye iliyokuwa nafasi yake kabla hajajiuzulu miaka miwili iliyopita.
CEO wa sasa Imani Kajula anatajwa kuomba kuondoka kwenye timu hiyo baada ya msimu kumalizika huku Rais wa heshima na mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji akivutiwa zaidi kufanya kazi na Barbara.