BARCA YAVUNJA REKODI YA MIAKA 100: Yafunga mabao 33 ndani ya mechi 7
Eric Buyanza
September 17, 2026
Share :

FC Barcelona imeweka rekodi mpya ya kihistoria baada ya kufunga jumla ya mabao 33 katika mechi saba za kwanza za msimu wa 2026–27. Kufuatia ushindi mnono wa mabao 7-2 dhidi ya Racing Santander, kikosi cha kocha Hansi Flick kimeshinda mechi zote saba. Huu unakuwa mwanzo bora zaidi wa ufungaji katika karne hii tangu klabu hiyo ilipoanzishwa.
Ingawa hii ni mara ya kwanza kuvunja rekodi hiyo katika soka la kisasa, kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kuwa Barcelona haijawahi kuwa na mwanzo hatari namna hii kwa zaidi ya karne moja. Mara ya mwisho kwa klabu hiyo kushinda mechi saba za kwanza na kufunga mabao mengi namna hii ilikuwa msimu wa 1915–1916, ambapo walifunga mabao 44 chini ya kocha Jack Greenwell.
Mfumo wa ushambuliaji wa Hansi Flick, unaojulikana kama "FlickBall," umeigeuza Barcelona kuwa mashine ya mabao.





