pmbet

Barcelona kumuongezea mkataba Hans Flick.

Joyce Shedrack

May 8, 2026
Share :

Klabu ya Barcelona inatarajia kumpa mkataba mpya kocha wake Hans Flick mara baada ya derby dhidi Real Madrid Jumapili hii, mchezo ambao endapo watashinda watakuwa mabingwa wa La Liga msimu wa 2025/2026.

Hansi Flick: Did you know?

Iwapo Barcelona watatwaa ubingwa Jumapili, wachezaji na wafanyakazi wameratibiwa kufanya gwaride la mjini humo Jumatatu kusherehekea ubingwa wa ligi na mashabiki, kama walivyofanya msimu uliopita baada ya kushinda mataji matatu ya nyumbani.

 

Wakala Pini Zahavi, anayemwakilisha Flick na Robert Lewandowski, aliwasili Barcelona Jumatano iliyopita na kuanza mzunguko wa mawasiliano siku ya Alhamisi juu ya mambo ya mikataba.

 

Mapema asubuhi hiyo, Rais mteule Joan Laporta alimtembelea Zahavi kwenye hoteli yake huko Passeig de Gracia na kukutana naye kwa zaidi ya saa tatu.

 

Mkutano huo ulilenga kukamilisha maelezo ya mkataba mpya ambao utamweka Flick Barcelona hadi Juni 2028, na mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 2027.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet