pmbet

Barcelona na Man City kwenye vita za kuiwania saini ya Dani Olmo

Eric Buyanza

April 18, 2024
Share :

Barcelona na Manchester City wanaripotiwa kuwa miongoni mwa vilabu vinavyowania kumsajili Dani Olmo wa RB Leipzig na taarifa zinasema tayari timu hizo zimeshafanya mazungumzo na mwakilishi wake.

 

Fowadi huyo wa RB Leipzig amekuwa bidhaa yenye thamani kutokana na uchezaji wake akiwa na kikosi hicho cha Bundesliga na hasa pia kutokana umahiri wake anapokuwa na timu ya taifa ya Uhispania.

Kulingana na gazeti la Daily Mail, klabu nyingi zimekuwa zikifuatilia nyendo za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Olmo alisaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Bundesliga Juni mwaka jana utakaoisha mwaka 2027. 



 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet