Barcelona wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumgombea Rodri
Eric Buyanza
August 6, 2026
Share :

Barcelona wameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili Rodri kutoka Manchester City.
Uamuzi huu wa Barcelona umekuja kufuatia taarifa za jeraha la muda mrefu la kiungo wao Frenkie de Jong, hali iliyowalazimu kutafuta mbadala wa kiwango cha juu.
Viongozi wa miamba hiyo ya Catalonia tayari wamefanya mawasiliano ya awali na wasaidizi pamoja na wawakilishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
Mbali na Barcelona, klabu za Real Madrid na PSG nazo ziko kwenye kinyang'anyiro hicho zikifuatilia kwa karibu hali yake.
Ripoti za karibu zinasema kuwa ingawa Rodri anavutiwa na mradi wa Barcelona, lakini chaguo lake la kwanza na la kipaumbele namba moja bado ni Real Madrid.





