Barcelona wamtambulisha Hans Flick kuwa mrithi wa Xavi
Sisti Herman
May 29, 2024
Share :
Klabu Barcelona ya ligi kuu nchini Hispania imemthibitisha kocha wa zamani wa Bayern Munich Hansi Flick kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili.
Flick, ambaye alitimuliwa na Ujerumani mnamo Septemba 2023, anachukua nafasi ya Xavi, ambaye alitimuliwa wiki iliyopita.
Msimu wa Flick akiwa na Ujerumani ulikuja baada ya kuiongoza Bayern Munich kushinda mataji matatu mwaka 2020, na kushinda Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski, alicheza chini ya Flick katika uwanja wa Allianz Arena kwa misimu miwili.
Bayern Munich ya Flick ilikamilisha msimu wa 2020 kwa kushinda Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa.