Barcelona yamsaini kinda wa Misri, Hamza Abdelkarim
Eric Buyanza
June 23, 2026
Share :
Klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Misri Hamza Abdelkarim kwa kandarasi ya miaka 3, kwa ada ya Euro milioni 1.5.
Hamza msimu uliopita ambao alikaa na timu za vijana na akiba za klabu hiyo, alionyesha uwezo mkubwa na kuishawishi sio Barcelona tu kumbakisha lakini pia kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, kumuita kwenye kikosi chake.
Abdelkarim mwenye umri wa miaka 18, tayari ameshacheza mechi zote mbili ambazo timu yake imecheza hadi sasa, ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya New Zealand, ambao ulikuwa ushindi wa kwanza kabisa kwa timu hiyo ya Kaskazini mwa Afrika katika Kombe la Dunia.






