pmbet

Barcelona yatwaa ubingwa wa 7 mfululizo wa ligi wakiiangusha Chelsea.

Joyce Shedrack

April 23, 2026
Share :

Klabu ya Wanawake wa Barcelona wamefanikiwa kushinda taji la 11 la ligi kuu katika historia ya klabu ikiwa ni taji la saba mfululizo wakiongeza pengo dhidi ya Athletic Club, wapinzani wao wa karibu wenye mataji matano ya ligi.

Barça Women claim their seventh league title in a row

Ubingwa huo walioutwaa rasmi usiku wa jana umewafanya Wanawake wa Barça sasa kuweka rekodi ya timu ya pili ya kushinda mataji ya ligi mfululizo katika ligi kuu za Ulaya, wakivunja rekodi ya Chelsea FC Women ya mataji sita mfululizo huku Olympique Lyonnais Féminin ikiwa kinara wa orodha hiyo wakiwa wametwaa taji la ligi ya Ufaransa mara 14 mfululizo kati ya 2006 na 2020.

 

Msimu huu ni mara ya sita wanatwaa taji la ligi wakiwa wamefunga zaidi ya mabao 100. Mwaka 2020/21 walifikia jumla ya mabao 167, kisha 159 (2021/22), 137 (2022/23), 118 (2023/24), 137 (2024/25) na 116 hadi sasa msimu huu huku zikiwa zimesalia mechi tano.

 

Mbali na ubora wao wa kushambulia, Barça pia wamekuwa bora kiulinzi, kwani huu ni ushindi wao wa saba mfululizo wa ligi wakiruhusu mabao 15 au chini yake.

 

Kiungo wa klabu hiyo Alexia Putellas ameendelea kuweka rekodi ya aliyeshinda mataji mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote katika kikosi akiwa na mataji tisa, akifuatiwa kwa karibu na gwiji mwingine wa blaugrana, Aitana Bonmatí mwenye mataji saba.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet