pmbet

Baridi ya Njombe inaathiri afya na uchumi

Sisti Herman

July 22, 2025
Share :

 

Hali ya baridi imeathiri afya na uchumi wa baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Njombe.

Baridi katika mkoa huo inaongeza magonjwa yanayohusiana na mazingira ya baridi na imeathiri baadhi ya biashara ikiwemo ya bodaboda.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Dk Jagadi Ntugwa alisema kipindi cha baridi husababisha kupungua kwa kiwango cha unywaji wa maji hivyo kuchangia ongezeko la magonjwa yakiwemo ya mawe kwenye figo kutokana na upungufu wa maji mwilini.

“Katika kipindi hiki, watu hupungukiwa na kiu, hivyo hawanywi maji ya kutosha, hali inayosababisha figo kushindwa kufanya kazi ipasavyo,” alisema Dk Ntugwa.

Katika maeneo mengi ya Njombe, familia hutumia moto wa mkaa ndani ya nyumba ili kujikinga na baridi.

Kufanya hivyo kunatajwa kuwa na madhara kwa afya ya binadamu hasa watoto na wazee ambao hupatwa na magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet