BASATA yazipiga kalenda tuzo za muziki 2025.
Joyce Shedrack
December 13, 2025
Share :
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kuahirisha kwa hafla yaugawaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2025, ambayo mwanzo ilikuwa imepangwa kufanyika leo tarehe 13 Desemba 2025.
Kupitia taarifa iliyochapishwa ukurasa wa Instagram wa BASATA imeeleza kuwa uamuzi wa kuahirisha umechukuliwa huku tarehe mpya ya hafla hiyo ikitarajiwa kutangazwa baadaye.
BASATA pia imewaomba radhi wasanii, wadau wa muziki na mashabiki wote kwa usumbufu wowote uliotokana na mabadiliko hayo.
“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea. Tunawaarifu kuwa hafla ya TMA iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 13/12/2025 imeahirishwa mpaka pale tarehe nyingine itakapotangazwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.





