Basi jipya la Simba kutoka kwa JayRutty kuwasilini Nchini hivi karibuni.
Joyce Shedrack
December 19, 2025
Share :
Baada ya ukimya wa muda mrefu kuhusu Basi la Simba SC waliloahidiwa na Mdhamini wake wa Jezi Jayrutty, Simba SC imesema basi hilo liko njiani linakuja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Clecentius Magori amesema ameona picha za badi hilo ambalo sasa linafanyiwa Branding.
“ Kuna mambo yanachekesha, lakini wacha niwatoe hofu. Simba SC basi liko na binafsi nimeona picha za basi hilo , alafu presha inatoka wapi wakati huyu mtu tuna mkataba nae wa Miaka 6.





