pmbet

Basi la Abood lakamatwa likiwa na dawa za kulevya

Sisti Herman

April 15, 2026
Share :

 

Basi la Abood lakamatwa likiwa na dawa za kulevya, zilifichwa kwenye mfumo wa hewa

BASI la abiria aina ya Yutong linalomilikiwa na kampuni ya Abood, lenye namba ya usajili T 181 EMJ, limekamatwa likiwa limebeba kilogramu 101.2 za dawa za kulevya aina ya mirungi katika eneo la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Aprili 13,2026 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Ukamataji huo, Kamishna Jenerali Lyimo amesema, ni matokeo ya operesheni kabambe iliyoendeshwa na DCEA katika kipindi cha mwezi Machi, 2026,

Amesema kuwa,basi hilo lilikuwa likifanya safari kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania ambapo dawa hizo zilikuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa katika maeneo mbalimbali ya chombo hicho cha usafiri, ikiwemo ndani ya mfumo wa hewa (AC), kwa lengo la kukwepa kugundulika.

Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali Lyimo, watuhumiwa waliokamatwa katika tukio hilo ni dereva wa basi hilo, Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39), ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet