Basi la Biashara Utd lavamiwa Tabora wachache wajeruhiwa.
Sisti Herman
June 16, 2024
Share :
Inaarifiwa kuwa Gari la Biashara United lilokuwa linaenda kwenye Kikao Cha Maandalizi ya mchezo (Pre Match Meeting) limeshambuliwa na wanaodaiwa ni Mashabiki wa Tabora United.
Taarifa zinadai kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Biashara United Mzee Omari Madenge amejeruhiwa vibaya eneo la Kichwani na amekimbizwa hospital kwaajili ya Matibabu.
Wachezaji wa Biashara Utd wapo Salama Kwasababu hakuwa miongoni mwa waliokuwepo kwenye basi hilo.
Biashara Utd wapo mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa Pili wa play off dhidi ya Tabora Utd unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi majira ya saa Kumi Jioni Leo.
Mechi ya Mkondo wa kwanza ambayo ilifanyika katika Uwanja wa CCM Karume , Biashara United waliibuka na Ushindi wa 1-0.