Basi la Tanzania lakamatwa likiwa na chatu Kenya
Sisti Herman
April 22, 2026
Share :

Nyoka aina ya Chatu amekutwa ndani ya basi la kampuni ya Kidia One, lililokuwa likifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Nairobi, siku ya Aprili 21, 2026.
Taarifa za awali, zinasema kuwa chatu huyo alikutwa akiwa amehifadhiwa ndani ya boksi, hali iliyozua taharuki kwa abiria wa basi hilo.
Hata hivyo, nyoka huko alichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa na maofisa wa hifadhi kutoka Shirika la Huduma za Wanyamapori la Kenya (KWS).
Tukio hilo linakuja miezi mitatu baada ya shehena ya bangi kupatikana ndani ya basi la kampuni hiyo hiyo, katika mpaka wa Namanga.





