pmbet

Basi laanguka darajani na kuteketea kwa moto, 45 wapoteza maisha

Eric Buyanza

March 29, 2024
Share :

Huko nchini Afrika Kusini basi la abiria linaloaminika lilikuwa likitokea nchini Botswana limeacha njia na kudondoka kutoka kwenye daraja la Mmamatlakala na kuteketea kwa moto na kuua watu 45 kati ya 46 waliokuwa ndani ya basi hilo, wizara ya uchukuzi ilisema.
 

Mamlaka ya mkoa wa kaskazini wa Limpopo imesema watu waliokuwa kwenye basi hilo walikuwa waumini waliokuwa wakielekea kwenye tamasha la Pasaka. Mtu pekee aliyenusurika katika ajali hiyo ni mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu.
 

Inadaiwa kuwa dereva alishindwa kulidhibiti gari hilo na hivyo kugonga vizuizi vya daraja na kuanguka korongoni.
 

Shughuli za uokoaji zinaendelea, lakini mamlaka eneo hilo imesema miili imeharibiwa vibaya kwa moto kiasi cha kutotambulika, na bado imenasa ndani gari hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet