pmbet

Basi latumbukia mtoni, takriban watu 10 wafariki

Eric Buyanza

May 22, 2024
Share :

Takriban watu 10 wamefariki dunia baada ya basi dogo kudondoka kwenye mto Nile, kaskazini mwa jiji la Cairo nchini Misri jana.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Misri, Hossam Abdelghaffar, aliiambia AFP. Idadi ya waliokufa ni 10, na inaweza kuongezeka.

Kwa mujibu wa Gazeti la Al-Ahram ambalo lilikuwa la kwanza kuripoti ajali hiyo, basi hilo dogo lilidondoka kutoka kwenye kivuko (pantoni) kilichokuwa kinavuka mto baada ya dereva wa basi hilo kutoweka breki ya mkono (Hand Brake), hata hivyo dereva huyo alikamatwa baada ya kujaribu kukimbia. 

Waziri wa Kazi wa Misri, Hassan Shehata, amesema basi hilo dogo lilikuwa likisafirisha wanawake wanaofanya kazi shambani, kulingana na Gazeti la Al-Ahram.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet