pmbet

Basi lawaka moto baada ya hitilafu ya breki

Sisti Herman

October 19, 2026
Share :

 

Taharuki imeibuka kwa abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Baraka Classic jijini Dar es Salaam baada ya basi hilo kushika moto.

Basi hilo lililokuwa safarini kutoka Mtwara kuelekea Dodoma, limeshika moto saa 1 asubuhi ya leo Jumatatu Oktoba 19, 2026.

Tukio hilo limetokea jijini Dar es Salaam, Barabara ya Mandela eneo la Tabata Mwananchi na kusababisha taharuki na hofu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Akieleza chanzo cha moto huo, dereva wa basi hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, ameeleza chanzo cha moto huo ni hitilafu ya breki ambayo umesababisha msuguano iliyosababisha moto kutokea.

"Breki zimejamu moto ukawaka, na sasa (saa 1 asubuhu) tunapambana kuuzima na tumewasiliana na mafundi wetu wanakuja kuangalia na kurekebisha tatizo tuendelee na safari," amesema.

Amefafanua matukio ya magari kushika moto si ya ajabu hasa ikiwa hitilafu ipo kwenye mfumo wa breki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet