pmbet

Basketball Tanzania yatwaa tuzo ya Dunia

Sisti Herman

December 31, 2023
Share :

Katika Mkutano wa Dunia wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (FIBA) uliofanyika Manila (Ufilipino) mwezi Agosti 2023 ulitoa Tuzo za FIBA ​​kwa Mashirikisho ya Kitaifa yaliyofanya vizuri kwa kipindi cha muda mfupi.

Kupitia mkutano huo, Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limepokea Tuzo ya kimataifa ya FIBA kwa Timu ya Wasichana iliyofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka 2021-2023 (Under 18 category).

Kupitia mtandao wao wa kijamii shirikisho la mchezo huo limeandika;

"Kwa kweli ni jambo la kujivunia kwa Nchi na TBF na wanamichezo wote kwa ujumla kwa mara ya kwanza kupata Tuzo ya Kimataifa kwa mchezo wa kikapu nchini.

"Hakika halikuwa jambo jepesi ndani ya kipindi cha miaka miwili tu ya uongozi kuweza kupata mafanikio haya makubwa. Msingi mkuu wa upatikanaji wa tuzo hii umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Shule ya Sekondari ya Orkeeswa ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kwenye maandalizi ya Kambi ya Timu ya Taifa ya Wanawake (U18) ikisimamiwa na Peter Louis (Meneja) , Raymond Yusuf Ngezi (Kocha) na Moreen Sizya (Kocha Msaidizi).

"Kwa namna ya pekee tunatoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Mama Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kutupatia msaada mkubwa kupitia Wizara ya Michezo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwa kuiwezesha timu hii kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na hatimaye kuweza kupata tuzo hii.

"Pia tunawashukuru viongozi wote wa TBF, mikoa, waandishi wa habari, mashabiki na wadau wote ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa sehemu ya kuwezesha upatikanaji kwa tuzo hii.

"Mwisho menejimenti ya TBF inatoa shukrani kwa wachezaji wa Timu ya Taifa (U18) ya wanawake kwa juhudi zao na umakini mkubwa katika ushiriki wao kwenye mashindano ya kimataifa na hatimaye kupatikana kwa tuzo hii".

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet