pmbet

BASSIROU FAYE: Kutoka gerezani mpaka kushinda Urais wa Senegal

Eric Buyanza

March 26, 2024
Share :

Mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuapishwa kuwa rais wa Senegal baada ya mpinzani wake mkuu kutoka chama tawala kukubali kushindwa, kufuatia uchaguzi uliofanyika siku 10 tu baada ya mshindi huyu wa Urais Bwana Bassirou Faye kuachiliwa huru kutoka gerezani alikokuwa akishikiliwa kwa makosa ya kisiasa na kwenda moja kwa moja kugombea nafasi hiyo ya juu kwenye Taifa.

Miezi michache tu iliyopita, Bwana Faye alikuwa amekaa kwenye chumba cha gereza na hakuwa akifahamika sana, lakini kila kitu kilikuja kubadilika wakati kiongozi wa chama chake, Ousmane Sonko aliponyimwa kugombea Urais akituhumiwa kwa uasi, hali iliyomfanya ampendekeze msaidizi wake wa karibu Bw Bassirou Faye agombee.

Akitumia kivuli na umaarufu wa bosi wake Ousmane Sonko, Bwana Faye jana Jumatatu (siku yake ya kutimiza miaka 44 ya kuzaliwa kwake) akafanikiwa kuibuka mshindi wa kiti cha Urais wa nchi hiyo na hivyo kumfanya mgombea wa upinzani wa kwanza kushinda kiti cha Urais tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet