Bayer Leverkusen hawazuiliki Ulaya, wafikisha 'Unbeaten' 47
Sisti Herman
May 3, 2024
Share :
Baada ya jana kushinda 2-0 mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya Uefa Europa Cup ugenini dhidi ya AS Roma, Mabingwa wa Bundesliga Bayer Leverkusen wamefikisha michezo 47 msimu huu kwenye mashindano yote bila kufungwa, ikiwa ni rekodi mpya baada ya kufikia rekodi ya michezo 46 ya Juventus bila kufungwa.
Bayer ambao hadi sasa bado wanashindania makombe mawili kati ya matatu inayopigiwa chapuo kuyabeba, inahitaji sare au ushindi wowote nyumbani ili kutinga fainali ya Europa League au kama watafungwa wasifungwe zaidi ya goli moja.
Pia Bayer wapo fainali ya DFB Pokal na watacheza dhidi ya Kaiserslautern ya ligi daraja la kwanza lakini pia wamebakisha michezo mitatu tu ya Bundesliga.
Je watamaliza msimu na 'Unbeaten' yao?