Bayern kumtimua Tuchel mwishoni mwa msimu
Sisti Herman
February 21, 2024
Share :
Ndoa ya klabu ya Bayern Munchen na kocha wao mkuu Thomas Tuchel itafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu mara baada ya majadiliano ya ndani kufikia umauzi huo kutokana na matokeo mabaya mfululizo ya timu hiyo hadi sasa kwenye mashindano yote.
“Tumekubaliana kwamba tutafikia ukomo wa ushirikiano wetu mwishioni mwa msimu huu na kutoka sasa hadi kufikia hapo mimi na jopo la wasaidizi wangu tutahakikisha tunaendelea kufanya kila kitu kwaajili ya kufikia mafanikio makubwa ya timu” alisema Tuchel.
Bayern ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Ujerumani ikiachwa alama 8 na vinara Bayer Leverkusen huku kikosi hicho cha Bavarians kikitoka kupoteza michezo mitatu mfululizo ya mashindano yote.
Bayern itaangalia uwezekano wa kutafuta na kumtangaza kocha mpya kwenye miezi 3-4 ijayo.