Bayern Munich wanaamini wataipata saini ya Bruno
Eric Buyanza
May 15, 2024
Share :
Bayern Munich wameonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United, Bruno Fernandes kwenye dirisha kubwa la usajili.
Munich wanaamini itakuwa rahisi kwao kupata huduma ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno hasa kutokana msimu mbaya inayopitia Manchester United.
Mustakabali wa Fernandes umekuwa na uvumi mkubwa tangu iliporipotiwa kwamba United iko tayari kusikiliza ofa kwa kila kiungo kando na Rasmus Hojlund, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho.