pmbet

Bayern Munich wanahusishwa na kumnunua Rashford

Eric Buyanza

July 2, 2025
Share :

Bayern Munich wameripotiwa kujiunga na mbio za kuisaka huduma ya Marcus Rashford kutoka Manchester United. 

Mtangazaji Christian Falk anasema kwamba Bayern "wana nia ya dhati" kwa Rashford na anadhani yuko kwenye orodha ya nyota wanaowindwa mno na klabu hiyo. 

Kwa upande wa Man U, wanataka dau la pauni milioni 40 kwa Rashford lakini wanaweza kuwa tayari pia kumruhusu kuondoka kwa mkopo kwa mara nyingine tena.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo akiwa na Aston Villa. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet