Bayern Munich yaweka mezani Pauni milioni 50 za kumnyakua Bernardo Silva
Eric Buyanza
June 24, 2024
Share :
Bayern Munich wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 50 kwa ajili ya kumnunua kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Bernardo Silva.
Silva amehusishwa mara nyingi sana na Barcelona, lakini ni wababe hao wa Ujerumani ambao wanatajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuipata saini yake iwapo ataamua kuondoka Etihad.