Bayern na Madrid, Kivumbi leo Uefa
Sisti Herman
April 30, 2024
Share :
Nusu fainali ya kwanza ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL) itachezwa leo ambapo klabu ya Bayern Munich watawakaribisha mabingwa wa kihistoria wa Uefa Real Madrid kwenye dimba la Allianz Arena leo usiku.
Real Madrid waliwatoa Manchester City huku Bayern wakiwaondosha Arsenal.
Bayern na Madrid kwenye Uefa CL wamekutana mara 16, Madrid ameshinda mara 9 huku Bayern akishinda mara 4 tu.